Tokyo. Kimbunga Nabi chaikumba Japan.
6 Septemba 2005Matangazo
Kimbunga Nabi kimesababisha watu kadha wamekufa ama kupotea nchini Japan.
Kimbunga Nabi kimeikumba pwani ya kusini ya kisiwa cha Kyushu na kinaelekea upande wa bahari ya Japan.
Safari kadha za ndege zimefutwa na waziri mkuu Junichiro Koizumi amesitisha kampeni za uchaguzi katika kisiwa cha Kyushu.
Kiasi cha watu 300,000 hawana umeme. Kimbunga Nabi kinasafiri kwa kasi ya kilometa 126 kwa saa. Hivi sasa kimepungua nguvu zake , lakini kimesambaa katika eneo kubwa.