1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tokyo. Kimbunga Nabi chashambulia kusini ya Japan.

6 Septemba 2005

Maeneo ya kusini mwa Japan yanaeshambuliwa na kimbunga Nabi.

Eneo ambalo limeathirika na kimbunga hicho ambacho kina upepo unaosafiri kwa kasi ya kilometa 144 kwa sasa na mvua kubwa ni kisiwa kilichoko katika eneo la kusini kabisa ya Japan cha Kyushu.

Polisi wanasema kuwa mwanamke mmoja amekufa maji baada ya kuanguka kutoka katika feri.

Watu karibu watano hawajulikani waliko hadi sasa.

Kasi ya kimbunga hicho imesababisha miji iliyoko karibu na bahari kufurika maji na kulazimisha mamia kwa maelfu ya wakaazi kuondolewa.

Magari hayatembei na usafirishaji umekwama , na kusababisha wasafiri wengi kushindwa kufanya safari zao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW