TOKYO: Kitabu cha historia kimesabisha maandamano
12 Aprili 2005Matangazo
Serikali ya Japani imesema imeingiwa na wasi wasi mkubwa kufuatia maandamano yaliofanywa dhidi ya Wajapani nchini Uchina mwishoni mwa juma.Maandamano hayo yalifanywa baada ya wizara ya elimu ya Japani kuidhinisha kitabu kipya cha historia ambacho wakosoaji wanasema kinaficha ukatili uliotendwa na Wajapani nchini Uchina wakati wa vita vikuu vya pili.Beijing imeihimiza Tokyo ijitahidi zaidi kurekebisha uhusiano wao.Maandamano dhidi ya Japani yalifanywa katika miji mbali mbali nchini Uchina mwishoni mwa wiki.Mjini Beijing na katika miji miwili kusini mwa nchi maandamano hayo yaliishia kwa machafuko.Ubalozi wa Japani mjini Beijing na maduka mengi na taasisi za Kijapani ziliharibiwa.