TOKYO: Koizumi aomba msamaha
15 Agosti 2005Waziri mkuu wa Japan, Junichiro Koizumi ameomba msahama kwa hatua ya Japan kuvamia na kuyakalia mataifa ya Asia katika sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya kushindwa kwa Japan katika vita vya pili vya dunia.
Koizumi amesema Japan haitasahau mafunzo yaliyojitokeza katika vita hivyo na kuelezea masikitiko makubwa kwa uharibifu uliosababishwa na Japan wakati wa vita hivyo.
Mawaziri wawili wa Japan wanajiandaa kuzuru makaburi ya wahanga waliouwawa wakati wa vita vya pili vya dunia. Waziri mkuu Koizumi, hatarajiwi kutoa heshima zake katika makaburi ya Yasukini, mahala ambapo wafungwa wa kivita pamoja na raia milioni 2.5 wa Japan watakumbukwa.
Wadadisi wanasema iwapo Koizumi atayatembelea makaburi hayo, hatua hiyo itazusha hasira kwa China na Korea Kusini, ambako wengi wanaamini Japan bado haijachukua dhamana kwa maovu iliyoyafanya wakati wa vita hivyo hata licha ya viongozi wake kuendelea kuomba msamaha mara kwa mara.