Tokyo. Kumbukumbu ya shambulio la bomu la kwanza la kinuklia kutumika katika vita imefanyika leo.
6 Agosti 2005Mataifa kadha duniani yamefanya kumbukumbu ya miaka 60 tangu pale lilipofanyika shambulio la bomu la kinuklia dhidi ya mji wa Hiroshima nchini Japan.
Hapo August 6, 1945 ndege ya kivita ya Marekani iliangusha bomu la kwanza la Atomic lililotumika katika vita, na kuua zaidi ya watu 140,000.
Mjini Hiroshima , watu walisimama kimya kwa muda ilipofika saa mbili na robo asubuhi kwa saa za Japan , wakati ambapo bomu hilo lilipolipuliwa.
Mamia kwa maelfu ya watu walitembelea katika eneo la kumbukumbu ya amani ya Hiroshima kwa ajili ya tukio hilo la kumbukumbu, ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi.
Bwana Koizumi amesema kuwa Japan ina nia thabiti ya kutafuta amani na kupinga silaha za kinuklia.
Hapo August 9, 1945, ndege nyingine ya kijeshi ya Marekani iliangusha tena bomu jingine katika mji wa Nagasaki, na kuua watu 80,000.