1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO : Mjukuu wa kwanza wa kiume azaliwa katika ufalme

6 Septemba 2006

Binti mfalme Kiko wa Japani leo amejifunguwa mtoto wa kiume.

Mtoto huyo anakuwa mrithi wa kwanza wa kiume kwa ufalme kuzaliwa katika kipindi cha miongo minne.Afisa wa Wakala wa Masuala ya Ufalme amewaambia waandishi wa habari mjini Tokyo kwamba Kiko amejifunguwa kwa opereseheni na kwamba mtoto wake alikuwa na uzito wa kilo 2 na nusu.

Shirika la habari la Kyodo limekariri duru zikisema mama pamoja na mtoto wote wako katika hali nzuri.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW