TOKYO: Rice amewasili Korea ya Kusini
19 Machi 2005Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amewasili Korea ya Kusini kwa ziara ya siku mbili.Suala la Korea Kaskazini linatazamiwa kuchukua sehemu kubwa ya mazungumzo yake.Alipozungumza katika Chuo Kikuu mjini Tokyo nchini Ujapani,Rice alitoa wito kuwa Korea ya Kaskazini moja kwa moja irejee kwenye majadiliano yanayohusika na miradi yake ya kinuklia.Kwa mara nyingine tena amesema Marekani "haina azma ya kuishambulia au kuivamia Korea ya Kaskazini." Akaongezea kuwa Washington ipo tayari kuihakikishia Korea ya Kaskazini usalama wake kwa kuzihusisha pande mbali mbali,ikiwa itaachilia mbali mpango wake wa kinuklia.Pyongyang imekataa kuendelea na majadiliano na Washington,ikimtaka Rice aombe msamaha kuhusika na matamshi kuwa Korea ya Kaskazini ni "ngóme ya udhalimu."Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na Rice barani Asia tangu kushika madaraka kama waziri wa kigeni wa Marekani.