TOKYO: Satalaiti ya nne ya Japan kuzunguka angani
24 Februari 2007Matangazo
Japan imerusha angani satalaiti yake ya nne ya upelelezi na hivyo kuiwezesha nchi hiyo kuchunguza harakati za sehemu mbali mbali duniani.Satalaiti hiyo pia itaimarisha uwezo wa Japan kufuatilia mradi wa nyuklia wa nchi jirani ya Korea ya Kaskazini.Roketi iliyobeba satalaiti hiyo ilirushwa Jumamosi mchana kutoka kituo kilicho kusini mwa nchi.Mwaka 1998 Japani iliamua kupeleka satalaiti 4 kuzunguka angani,baada ya Korea ya Kaskazini kurusha kombora kwenye kisiwa chake kikuu.