TOKYO: Sharon kuzuru Japan.
9 Machi 2005Matangazo
Waziri mkuu wa Israel Bwana Ariel Sharon ataizuru Japan baadaye mwezi May ama mapema mwezi wa Juni katika juhudi za kujadili hatua za amani ya mashariki ya kati pamoja na waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi.
Balozi wa Israel nchini Japan Bwana Eli Cohen amemwambia Bwana Koizumi kuwa Bwana Sharon atakuwa tayari kufanya ziara hiyo nchini Japan baada ya kumaliza ya kukamilisha masuala mengine yaliyokwisha pangwa kuanzia mwezi wa Aprili hadi May. Bwana Koizumi alimwambia Cohen kuwa Japan inataka kufanya kile inachofikiria kukifanya kwa ajili ya amani ya mashariki ya kati.
.