TOKYO: Shinzo Abe apelekwa hospitali kwa machofu
13 Septemba 2007Matangazo
Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe anaeondoka madarakani amepelekwa hospitali,siku moja baada ya kujiuzulu kwa ghafula.Kwa mujibu wa maafisa, Abe ana machofu,lakini vyombo vya habari nchini Japani vinasema,afya ya Abe imedhoofika tangu chama chake kushindwa vibaya sana katika uchaguzi wa bunge uliofanywa tarehe 29 mwezi wa Julai.