TOKYO: Tetemeko la ardhi nchini Japan
25 Machi 2007Matangazo
Tetemeko kubwa la ardhi lenye nguvu ya 7.1 kwenye Kipimo cha Richter,limetokea nchini Japan asubuhi ya leo.Idara ya kutabiri hali ya hewa imesema, mawimbi makubwa kama Tsunami yanatazamiwa kutokea kwenye pwani ya magharibi ya kisiwa kikuu cha Honshu.Japan ni miongoni mwa nchi ambako mitetemeko ya ardhi hutokea mara nyingi.