TOKYO: Uchaguzi wa baraza kuu la bunge nchini Japan
29 Julai 2007Matangazo
Wajapani leo wanapiga kura kuchagua baraza kuu la bunge.Uchunguzi wa maoni uliofanywa hivi karibuni umeashiria kuwa serikali ya Waziri Mkuu Shinzo Abe,itashindwa vibaya sana.Wadadisi wanasema,Abe huenda akashinikzwa na chama chake cha Liberal Demokratik ajiuzulu,pindi chama hicho kitapoteza wingi wa kudhibiti baraza hilo,licha ya kuwa na wingi katika baraza dogo bungeni.
Umashuhuri wa Abe umepunguwa kwa sababu ya kashfa mbali mbali,ikiwa ni pamoja na ile inayohusika na malipo ya pensheni ya uzeeni.