TOKYO: Virusi hatari vya H5N1 vimechomoza Japan
27 Januari 2007Matangazo
Uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa homa ya mafua ya ndege ilioripuka kusini mwa Japan kwenye shamba wanakofugwa kuku,imesababishwa na virusi hatari vya H5N1.Maafisa katika eneo hilo sasa wanasimamia utaratibu wa kuwaua kuku wote wapatao 50,000 katika shamba hilo, baada ya zaidi ya kuku 3,000 kufariki kutokana na ugonjwa huo.Vile vile kama hatua ya tahadhari,watawaua wengine 50,000 katika shamba lililo jirani.Kwa mujibu wa WHO-Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa,tangu mwaka 2003,watu 269 wameambukizwa na virusi vya H5N1 na 163 wamefariki katika sehemu mbali mbali duniani.