TOKYO: Wajapani leo wanachagua serikali za mitaa
8 Aprili 2007Matangazo
Wapiga kura nchini Japan hii leo wanapiga kura kuchagua serikali za mitaa.Chaguzi hizo ni mtihani wa kwanza wa serikali ya waziri mkuu Shinzo Abe,iliyoshika madaraka mwaka jana wakati wa majira ya mapukutiko.Wagombea kura wanapigania ugavana katika miji 14,ikiwa ni pamoja na mji mkuu Tokyo.Chaguzi hizo ni kipimo muhimu kwa serikali,kabla ya kufanywa chaguzi za bunge katika majira ya joto.