TOKYO: Wajapani wapiga kura katika uchaguzi mkuu
11 Septemba 2005Matangazo
Wajapani wanapiga kura zao katika uchaguzi mkuu ulioitishwa mapema na waziri mkuu Junichiro Koizumi.Uchaguzi huu unatazamwa kama ni kura ya maoni kuhusu mageuzi ya kiuchumi yaliyopendekezwa na Koizumi.Uchunguzi wa maoni unatabiri kuwa chama cha Koizumi cha Liberal Democratic Party, kitajipatia ushindi kwa urahisi.Tarehe 8 Agosti, Koizumi aliitisha uchaguzi kabla ya wakati,baada ya wapinzani katika chama chake,kufanikiwa kuupinga mpango wake wa kutaka kubinafsisha huduma za posta.