TOKYO: Wanajeshi wa Japan warejea nyumbani
25 Julai 2006Matangazo
Kikosi cha mwisho cha Japan kilichokuwepo nchini Irak,kimesharejea nyumbani baada ya kukamilisha operesheni muhimu kabisa ya kijeshi ya nchi hiyo tangu kumalizika Vita Vikuu vya pili.Wanajeshi 600 walishughulika na huduma za kiutu katika mji wa Samawa kusini mwa Irak na hawakuhusika na mapigano.