1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TOKYO. Waziri mkuu alivunja bunge

8 Agosti 2005

Waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi amelivunja bunge la nchi hiyo ili kufanyike uchaguzi wa mapema.

Uamuzi huo umetokana na hatua ya awali ya bunge la nchi hiyo kuupinga mswada wa waziri mkuu wa kutaka kubinafsisha huduma za shirika la posta.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wanachama 20 wa LDP chama cha waziri mkuu Koizumi ni miongoni mwa walioupinga mswada huo.

Naibu wa waziri mkuu katika muungano wa vyama Mseto nchini Japan bwana New Komeito amesema kuwa uchaguzi huenda ukafanyika septemba 11.

Bwana Junichiro Koizumi aliamini hatua ya kuzigawa huduma za posta katika awamu nne huenda ingekwamua uchumi wa Japan.

Shirika la posta la Japan lina rasilimali kufikia dola trilioni tatu na linatoa pia huduma za benki na za bima.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW