TOKYO: Waziri mkuu wa Irak azuru Japan
9 Aprili 2007Waziri mkuu wa Irak Nouri al Malik ameishukuru Japan kwa kuiunga mkono nchi yake katika juhudi za ujenzi wa taifa hilo na amewataka wamiliki wa makampuni kutoka Japan kurejesha tena shughuli zao za biashara nchini humo.
Bwana Malik alizungumza hayo alipokuwahutubia waandishi wa habari mjini Tokyo kabla ya kukutana na mfalme Akihito wa Japan.
Waziri mkuu wa Irak Nouri al Malik pia atakutana na waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Ndege ya bwana Al Malik ilichelewa kuwasili mjini Tokyo baada ya ndge hiyo kunyimwa ruhusa ya kuruka katika anga ya Iran.
Japan iliunga mkono operesheni iliyo ongozwa na Marekani ya kuivamia Irak mwaka 2003,ilitoa mchango wa wanajeshi wake katika mji wa kusini wa Samawah.
Hata hivyo Japan iliyaondoa majeshi yake kutoka Irak mwaka jana.