TOKYO;Ajiuzulu kwa kuunga mkono Japan kupigwa bomu la atomik
3 Julai 2007Matangazo
Waziri wa Ulinzi wa Japan Fumio Kyuma amejiuzulu kufuatia matamshi yake ya kwamba shambulizi la bomu la atomik la Marekani nchini Japan, lilikuwa ni njia ya lazima kumaliza vita kuu ya pili ya dunia.
Fumio aliwaambia waandishi wa habari mjini Tokyo ya kwamba Waziri Mkuu Shinzo Abe amekubalia kujiuzulu kwake.
Fumio hapo siku ya jumamosi aliibua ghadhabu miongoni mwa wajapan aliposema kuwa shambulizi hilo la Marekani nchini Japan lisingeweza kuepukika.