TOKYO:Bwana Koizumi achaguliwa tena kuwa Waziri Mkuu wa Japan.
21 Septemba 2005Matangazo
Mabunge yote mawili ya Japan yamemchagua kwa mara nyingine Bwana Junichiro Koizumi,kuendelea na wadhifa wake wa Uwaziri Mkuu wakati wa kikao maalum kilichofanyika leo.
Bwana Koizumi alichaguliwa kwa wingi wa kura pamoja na chama chake,ambapo sasa wanawabunge 340 kati ya wabunge 480 walio katika Bunge la Japan.
Chama cha Bwana Koizumi cha LDP,kilipata ushindi mnono katika uchaguzi mkuu aliouitisha mapema mwezi uliopita,ili kutafuta kuungwa mkono kutokana na mipango yake ya kuleta mageuzi na kubinafsisha mfumo wa shughuli za posta nchini Japan.