TOKYO:Waziri mkuu wa Japan Koizumi apata ushindi mkubwa
12 Septemba 2005Waziri mkuu wa Japan Junichiro Koizumi leo ameapa kuendelea na mpango wake wa mageuzi katika Posta ya Japan baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu nchini humo.
Chama cha waziri mkuu Koizumi LDP na washirika wake katika muungano kimejinyakulia viti 296 kati ya viti 480 vya bunge vilivyokuwa vikigombaniwa.
Chama cha upinzani kinachoongozwa na Katsuya Okada kimejipatia viti 113 pekee na hivyo basi kiongozi wa chama hicho amejiuzulu akisema kwamba ujembe wa chama hicho haukuwafikia wananchi.
Kwa upande wake waziri mkuu Koizumi amesema matokeo ya uchaguzi huo yameonyesha kuwa mpango wake wa kutaka kubinafsisha posta ya Japan unaungwa mkono na wengi nchini humo.
Koizumi aliitisha uchaguzi wa mapema baada ya bunge kuuzuia mswaada wa kubifsisha Posta ya Japan uliopendekezwa na Koizumi.