Tony Blair angátuka madarakani
27 Juni 2007Gordon Brown ambae hivi sasa ni waziri wa fedha atamrithi Tony Blair kama waziri mkuu mpya wa Uingereza.Muda mfupi baadae,inatazamiwa kuwa Tony Blair atatajwa kama mjumbe mpya wa ngazi ya juu wa kundi la pande nne linalohusika kutafuta suluhisho la mgogoro wa Mashariki ya Kati.Blair amekataa kusema cho chote kuhusu uvumi unaohusika na kuchagukliwa kwake,lakini alipozungumza na waandishi wa habari alisema:
„Yeyote anaejali amani na utulivu duniani, anafahamu kwamba azimio la kudumu,kuhusika na suala la Israel na Wapalestina ni muhimu. Akaongezea kuwa atafanya kila awezacho kusaidia kupata azimio la aina hiyo.
Kwa mujibu wa mjumbe wa Umoja wa Ulaya,Blair ni mtu pekee anaefikiriwa kwa wadhifa huo.Kundi la pande nne hujumuisha Umoja wa Ulaya,Umoja wa Mataifa,Urusi na Marekani.