1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TORONTO: Mkutano wa kimataifa kuhusu ukimwi waendelea nchini Canada

14 Agosti 2006

Mkutano wa kimataifa wa 16 kuhusu ukimwi unaendelea mjini Toronto Canada. Muanzilishi wa kampuni ya Microsoft, Bill Gates akitoa hotuba ya ufunguzi amesema atatoa fedha zaidi kudhamini utafiti wa ukimwi na kutafuta chanjo ya kuzuia maambukizi ya ukimwi.

Hata hivyo bwana Gates amezitaka serikali mbalimbali na wahisani wengine waongeze juhudi zao na kuchanga fedha zaidi. Amesisitiza juu ya umuhimu wa kutafuta njia bora zaidi za kuwawezesha wanawake kujikinga kutokana na ukimwi.

Shirika la Afya duniani, WHO, linakadiria kwamba nusu ya watu milioni 39 walioambukizwa ukimwi leo, ni wanawake. Zaidi ya wajumbe elfu 20 wanahudhuria mkutano wa mjini Toronto.