TORONTO; Ujerumani aahidi Euro milioni 400 kila mwaka kusaidia juhudi za kupambana na maradhi ya ukimwi
14 Agosti 2006Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani bibi Heidemarie Wieczorek Zeul amesema , kuanzia mwaka 2008 Ujerumani itatoa mchango wa Euro milioni mia nne kila mwaka ili kusaidia juhudi za kupambana na maradhi ya ukimwi.
Bibi Wieczeork Zeul amesema hayo kwenye mkutano wa kimataifa juu ya ugonjwa wa ukimwi mjini Toronto , unaohudhuriwa na wajumbe zaidi alfu 20 kutoka nchi 132.
Waziri huyo wa Ujerumani pia ametaka hatua thabiti zichukuliwe kwa lengo la kuwakinga wasichana na wanawake na maradhi hayo.
Akizungumza kwenye mkutano huo mwasisi wa kampuni ya Microsoft Bill Gates ambae ni mfadhili mkubwa wa mradi wa kupambana na ukimwi amesema ataendelea kuufadhili mradi wa utafiti na kinga ya maradhi hayo lakini pia amezitaka serikali na wafhadhili wengine nao wafanye zaidi.