1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tottenham, wafalme wa London?

7 Desemba 2020

Tottenham Hotspur wamerudi kileleni mwa ligi hiyo baada ya kuwazaba Arsenal magoli mawili kwa bila katika mechi iliyochezwa kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa mbele ya mashabiki elfu mbili wa Spurs.

England Premier League | Tottenham Hotspur v Southampton | Harry Kane
Picha: Reuters/E. Keogh

Baada ya kushindwa huko Arsenal kwa sasa wanaishikilia nafasi ya kumi na tano kwenye msimamo na katika mechi zao nne zilizopita wameshindwa tatu na kutoka sare ya kutofungana moja. Kocha wao Mikel Arteta anasema vijana wake walitimiza masharti yote aliyowapa katika mechi ya jana ila maji yalizidi unga tu.

Mabingwa Liverpool walipata ushindi wa magoli manne kwa bila walipokuwa wakicheza na Wolverhampton Wanderers na kwa sasa wako sawa kialama na Spurs ingawa Tottenham wamewazidi kwa wingi wa mabao.

Jumamosi ijayo mechi itakayotazamwa na wengi ni Manchester Derby uwanjanin Old Trafford ambapo Manchester United watakuwa wanakwaana na mahasimu wao Manchester City katika mechi itakayokuwa inapatanisha timu iliyo kwenye nafasi ya tano na sita kwenye jedwali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW