1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tozo, wasiwasi watawala kwa mabenki Tanzania

7 Septemba 2022

Tozo mpya zinazokatwa kwenye miamala ya kieloktroniki na serikali nchini Tanzania limezidi kuibua wasiwasi kwa mabenki kupoteza amana za wateja wanaotumia benki hizo kufanya miamala.

Afrika Tansania Finanzminister  Mwigulu Nchemba
Picha: Deo Kaji Makomba/DW


Suala la tuzo mpya zinazokatwa kwenye miamala ya kieloktroniki na serikali nchini Tanzania limezidi kuibua mjadala mkubwa huku wasiwasi ukianza kujitokeza kwa mabenki kupoteza amana za wateja wanaotumia benki hizo kufanya miamala. 

Tayari  Kampuni moja ya simu imetangaza kupata hasara ya mabilioni ya shilingi tangu tozo hizo zilipotangazwa. 

Wakati wananchi wakiendelea kunung’unika na kuhisi machungu ya tuzo hiyo, kampuni ya simu ya Vodacom imesema wateja wake zaidi ya milioni 1.3 wameacha kutumia huduma ya Mpesa kutokana na tozo na kwamba anguko hilo la wateja limeshuhudiwa tangu kulipoanzishwa tuzo kwenye miamala ya simu, Julai 15, 2021.

Kampuni hiyo ambayo hisa zake zimeorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam, imepoteza kiasi cha Shilingi bilioni 103.8, katika awamu ya kwanza ya mwaka 2022 iliyoishia Machi. 

Soma pia:TWAWEZA: Wananchi wana wasiwasi na kupanda gharama za maisha
kuletwa kwa tozo nyingine mpya ijulikanayo tozo ya miamala ya kieloktroniki kumezidisha wasiwasi wa uwezekano wa kuongezeka athari  katika sekta nyingine kama vile mabenki na sekta nyingine ikiwemo huduma za simu.

Kwa upande wananchi sehemu kubwa ya mijadala yao ni kuhusu tozo hiyo na kwambawengi wanaonekana kushitushwa kwa namna inavyokata miamala yao ya fedha.

 Serikali yatetea tozo mpya 
Waziri wa fedha Mwingulu Nchemba ametetea uamuzi huo wa serikali akisema tozo hiyo haijalenga kumbana mwananchi mbali ya kupanua vyanzo vya mapato kwa ajili ya kugharimia miradi ya maendeleo ya nchini.

Hata hivyo, tozo hiyo bado inaendelea kuzua mijadala na tayari kituo cha sheria na haki za binadamu kimefungua kesi katika mahakamu kuu ya Tanzania kikipinga ujio wake.

Soma pia:Kodi mpya ya miamala Tanzania yawatia wananchi wasiwasi
 Kulingana na afisa wa kituo  hicho, Wakili Madihiya ujio wa tozo hiyo umekiuka baadhi ya vipengele vya katiba ya nchi.

Baadhi ya wachambuzi wa masualaya uchumi na siasa wanasema,Bunge lijalo litakaloanza wiki ijayo, suala la tozo hiyo ikawa moja ya mijadala itayotawala kwa sehemu kubwa.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW