1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Treni mbili zagongana India na kusababisha vifo vya watu 7

17 Juni 2024

Polisi nchini India imesema watu 7 wameuwawa wakati treni ya abiria ilipogongana na ile ya mizigo Magharibi mwa jimbo la Bengal.Vidio zinaonyesha mabehewa ya treni hizo yakiwa yameanguka

Zoezi la uokoaji likiendelea baada ya ajali kutokea India
Zoezi la uokoaji likiendelea katika eneo la mkasa wa ajali ya treni ya abiria na mizigo huko India.Picha: Diptendu Dutta/AFP/Getty Images

Kulingana na afisa wa polisi katika eneo hilo la ajali, Iftikar-Ul-Hassan watu wengine 39 wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali iliyokuwa karibu. Ajali hiyo ya treni ni ya hivi karibuni kuikumba sekta hiyo ya usafiri inayotumiwa na mamilioni ya watu kila siku. 

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ametoasalamu zake za rambirambi kwa wale waliopoteza jamaa zao katika tukio hilo. Akiandika katika ukurasa wake wa kijamii Modi alithibitisha shughuli za uokozi bado zinaendelea.

Soma pia:India: Watu wanane wamekufa kufuatia ajali ya treni

Madaktari, magari ya kubebea wagonjwa na makundi ya kushughulikia majanga wamepelekwa katika eneo hilo kusaidia majeruhi.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW