1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Treni yachomwa moto Amsterdam wakati hali ikisalia tete

12 Novemba 2024

Polisi mjini Amsterdam Uholanzi, imesema mamia ya watu waliokuwa wamebeba fimbo na fataki, walichoma treni wakati jiji hilo likisalia katika hali ya sintofahamu kufuatia ghasia za wiki iliyopita

Maandamano ya Amsterdam
Treni yachomwa moto huko Amsterdam wakati hali ikiendelea kusalia tetePicha: TALHA ANDAC/ANP/AFP

Polisi walifanikiwa kuzima moto huo huku maafisa wa kushughulikia ghasia wakidhibiti eneo la mkasa.

Picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ziliwaonyesha watu wakiharibu mali na kuwasha fataki. Polisi wameeleza kwamba bado hawajafahamu walioanzisha ghasia hizo na kama zinahusiana na machafuko ya wiki iliyopita.

Israel yatuma ndege mbili kuwaokoa raia wake Amsterdam

Machafuko hayo ya wiki iliyopita yalitokea wakati wa mechi baina ya klabu ya Maccabi Tel Aviv na Ajax. Watu watano walijeruhiwa na wengine kadhaa kukamatwa kufuatia ghasia hizo. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW