1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI; adhabu ya kifo kucheleweshwa nchini Libya

15 Novemba 2005

Mahakama kuu nchini Libya imechelewesha uamuzi juu ya hukumu ya kifo kwa wauguzi wa nchi za nje waliopatikana na hatia ya kuwaambukiza watoto ugonjwa wa ukimwi.

Manesi watano kutoka Bulgaria na daktari mmoja wa kipalestina walihukumiwa adhabu ya kifo mwaka jana licha ya malalamiko kutoka Marekani na nchi za Umoja wa Ulaya.

Mahakama hiyo imesema imechelewesha uamuzi juu ya adhabu hiyo ili kutoa muda kwa upande wa utetezi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW