1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI : Gaddafi alaani azimio la Umoja wa Mataifa

3 Aprili 2005

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amelaani kura ya Umoja wa Mataifa inayotaka kufikishwa kwa Wasudan wanaotuhumiwa kwa uhalifu wa vita huko Dafur kwenye Mahkama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kuwa ni ukiukaji dhahiri wa uhuru wa Sudan.

Gaddafi amesema katika taarifa iliyorepotiwa na shirika la habari la taifa JANA hapo jana usiku kwamba sheria pekee za Sudan ndio zina haki ya kuwashtaki wananchi ndani ya Sudan. Amesema uamuzi huo wa Umoja wa Mataifa unakusudia kuchochea mzozo wa Dafur na hautosaidia kutatuwa mzozo huo.

Gaddafi ana mahusiano ya karibu na viongozi wa serikali ya Sudan na mahasimu wao waasi wa jimbo la Dafur.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW