TRIPOLI: Libya imeionya Marekani iondoe vikwazo ...
3 Januari 2004Matangazo
vya uchumi iliyoiwekea nchi hiyo itakapofika mwezi Mei mwaka huu,ama sivyo iwe tayari kukosa malipo ya fidia ya watu waliokufa katika ajali ya ndege ya mwaka 1988 liyoripuliwa kwa bomu.
Gazeti moja la Marekani la New York Times,limekariri taarifa za viongozi wa Libya zikiitaka Marekani kuchukua haraka hatua za kuiondolea nchi yao vikwazo vya uchumi hasa baada ya Libya kukubali kuachana na utengenezaji wa silaha za maangamizi na kuwaruhusu wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa kukagua mitambo yake ya kinulkia.
Libya imekiri kuhusika na kuangushwa kwa ndege ya Pan Am katika anga ya Lockerbie nchini Scotland mwaka 1988,ajali liyonyakua maisha ya watu 270.Wataalam wa nuklia wa Umoja wa Mataifa,wameeleza kupata ushirikiano mkubwa kutoka maofisa wa Libya,wakati walipokuwa wakitekeleza kazi yao ya awali ya ukaguzi nchini Libya.