1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tripoli: Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, AU, umemalizika mjini Sirte,Libya

6 Julai 2005

Nchi za Kiafrika zimezitaka nchi tajiri zinazoongoza kiviwanda duniani ziutekeleza kwa haraka mpango ulioshauriwa na Uengereza katika kuukomesha umaskini barani Afrika. Mwishoni mwa mkutano wa kilele uliofanyika Libya, nchi 53 za Umoja wa Afrika, AU, zimetaka utolewe msamaha wa madeni, yafanywe marekebisho katika mfumo wa biashara duniani na misaada zaidi itolewekatika kupambana na umaskini katika bara lao.Ripoti ya tume ilioundwa na waziri mkuu wa Uengereza, Tony Blair, itazungumziwa katika mkutano wa kilele unaoanza leo wa nchi nane tajiri duniani huko Scotland. Zaidi ya asilimia 40 ya wakaazi milioni 800 katika Afrika wanaishi kwa kutegemea kipato cha chini ya dala moja ya Kimarekani kwa siku; milioni 200 wanahatarishwa na utapio mlo na milioni mbili wanakufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa Ukimwi.

Licha ya suala la kuzifutia madeni nchi maskini sana, mkutano wa kilele wa Scotland utajishughulisha pia na usafir wa mazingira. Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kulinda Mazingira duniani, Klaus Töpfer, amewahimiza washiriki wachuwe hatua za kulinda misitu na fukwe za bahari. Alisema katika kuupiga vita umaskini, kuwa na maji safi ni jambo muhimu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW