1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aashiria vita na Iran vinaelekea mwisho

10 Machi 2026

Rais Donald Trump wa Marekani ameashiria kuwa vita vya Mashariki ya Kati vinaelekea ukingoni licha ya kuendelea kwa mashambulizi makali dhidi ya Iran na mashaka juu ya uthabiti wa uchumi wa dunia.

Miami, Florida, Marekani| Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani.Picha: Kevin Lamarque/Reuters

Akizungumza na waandishi habari huko Florida, Trump amesema Marekani ilichukua uamuzi wa kuishambulia Iran "kuusambaratisha utawala ulojaa uovu" lakini anaamini vita kwamba vilivyozuka havitakuwa vya muda mrefu.

Kiongozi huyo pia ameionya Iran dhidi ya hatua zozote za kuzuia biashara ya mafuta kupitia mlango bahari wa Hormuz ambao hupitisha kiasi asilimia 20 ya mafuta yote duniani.

Trump ametoa matamshi hayo wakati Israel iliendelea kuishambulia Iran usiku wa kuamkia leo. Tehran nayo ilivurumisha makombora ya masafa kuulenga mji wa Tel Aviv na miji ya mataifa kadhaa ya kanda hiyo ikiwemo Bahrain na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW