1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Trump achoshwa na mikutano isiyoleta mwanga wa amani Ukraine

12 Desemba 2025

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Karoline Leavitt amesema Donald Trump "amechoshwa na mikutano ya mara kwa mara" ambayo hadi sasa haijatoa mwanga wa kufikiwa kwa makubaliano ya kuvimaliza vita kati ya Urusi na Ukraine.

USA | Washington D.C. 2025 | Karoline Leavitt
Msemaji wa Ikulu ya Marekani Karoline LeavittPicha: Evan Vucci/AP Photo/dpa/picture alliance

Msemaji wa Ikulu ya Marekani Karoline Leavitt amesema Rais Donald Trump "amechoshwa na mikutano ya mara kwa mara" ambayo hadi sasa haijatoa mwanga wa kufikia makubaliano ya kuvimalita vita kati ya Urusi na Ukraine.

Ametoa kauli hiyo wakati Kyiv ikieleza kwamba Washington bado inaishinikiza ikubali mpango wake unaojumuisha kuachia baadhi ya maeneo yake kwa Urusi kama sehemu ya makubaliano ya kuvimaliza vita vilivyodumu takriban miaka minne.

Leavitt amewaambia waandishi wa habari kwamba Trump hataki tena kile alichokiita maneno matupu bila vitendo na kwamba anachotaka kuona sasa ni vita hivyo kufika mwisho.

Hivi karibuni, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa kauli iliyoashiria kwamba hakuna mabadiliko makubwa katika msimamo wa Marekani juu ya namna vita hivyo vinapaswa kumalizika tangu Washington ilipowasilisha mpango wake wa vipengele 28 mwezi uliopita - mpango ulioonekana kuipendelea zaidi Urusi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW