MigogoroMashariki ya Kati
Trump adai Iran inakaribia "kusalimu amri"
13 Machi 2026
Matangazo
Hayo yameripotiwa na shirika la habai la Ujerumani, dpa, likiwanukuu maafisa watatu wanaofahamu kilichojadiliwa ndani ya mkutano huo wa kundi la G7 uliofanyika leo kwa njia ya mtandao.
Mapema leo alfajiri Trump aliandika mtandaoni kuwa nguvu za kijeshi za Iran zimedhoofika na kwamba amedhamiria "kuwaua" viongozi wa Iran akiwaita "watu waovu" waliosababisha maafa tangu kuundwa kwa jamhuri ya kiislamu mwaka 1979.
Hapo jana Kiongozi Mkuu mpya wa Iran Ayatollah Mojtaba Khamenei alisema nchi yake ni lazima iendele kupambana dhidi ya Marekani na Israel na kuyatolea mwito mataifa jirani kuzifunga kambi za kijeshi za Marekani.