1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aendelea kuisaka kinga dhidi ya makosa yanayomkabili

Hawa Bihoga
20 Machi 2024

Rais wa zamani Donald Trump amewasilisha mukhtasari wa Mahakama ya Juu ya Marekani katika kupata kinga kutoka kwa wanendesha mashtaka kwa kujaribu kutengua matokeo ya uchaguzi wa 2020.

Marekani | Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akiwa katika moja ya mikutano yake ya kisiasa.Picha: Meg Kinnard/AP Photo/picture alliance

Kesi dhidi ya mwanansiasa huyo ikitarajiwa kutajwa mbele ya majaji mwezi ujao.

Trump anakata rufaa katika mahakama ya chini kukataa ombi lake la kinga dhidi ya kesi ya jinai inayofuatiliwa na Wakili Maalum Jack Smith kwa sababu alikuwa rais alipochukua hatua zilizolenga kubatilisha ushindi wa Rais Joe Biden dhidi yake.

Soma pia:Korti ya juu Marekani yakataa kumkinga mshauri wa Trump dhidi ya jela

Trump ambae ni rais wa kwanza wa zamani kufunguliwa mashitaka ya jinai, ni mgombea wa Republikani anayechuwana na Rais Joe Biden wa Kidemokratiki katika uchaguzi wa Novemba 5 ambao unavuta nadhari ya kimataifa.

Hata hivyo wafuatiliaji wa siasa za Marekani wanasema kuwa, iwapo Trump atarejea Ikulu ya White House anaweza kutumia mamlaka kufuta mashtaka dhidi yake.
 

Kwa habari nyingine za ulimwengu, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube