1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aendelea kuteua viongozi wapya wa serikali ijayo

12 Novemba 2024

Rais Mteule wa Marekani Donald Trump ameendelea kupanga safu yake ya uongozi kwa kufanya uteuzi wa viongozi wapya.

Uchaguzi wa Marekani 2024 | Chama cha Republican | Trump Donald J Trump
Rais mteule wa Marekani Donald J Trump Picha: Evan Vucci/AP Photo/dpa/picture alliance

Tajiri huyo wa chama cha Republican mwenye umri wa miaka 78,  amemtangaza Tom Homan kama mkuu wa uhamiaji na mipaka, akimtwika jukumu la kutimiza ahadi yake ya kuwatimua wahamiaji wasio na vibali.

Aidha, gazeti la New York Times, limeripoti kwamba Trump anatazamiwa kumteua Seneta wa Florida Marco Rubio kuwa waziri wa mambo ya nje huku Mike Waltz akitajwa kuwa atachukua nafasi ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Mike Waltz kuwa mshauri wa Usalama wa Taifa

Wote wawili wamekuwa na mitizamo hasi kuelekea China, ambayo wanaitizama kama tishio na changamoto kwa nguvu za kijeshi na kiuchumi za Marekani.

Trump pia tayari amemteua mbunge wa New York Elise Stefanik kushika wadhifa wa balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW