Trump afikiria kumaliza vita vyake Mashariki ya Kati
21 Machi 2026
Matangazo
Taarifa hizo za mkanganyiko za Marekani zinakuja baada ya kupanda tena kwa bei ya mafuta na hivyo kupelekea kushuka kwa soko la hisa la Marekani. Hayo yanafuatiwa pia na tangazo la utawala wa Trump kwamba utaondoa vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran yanayopakiwa kwenye meli, hatua inayolenga kukabiliana na ongezeko hilo la bei ya mafuta.
Hata hivyo, vita hivyo havijaonyesha dalili za kupungua licha ya Iran kusherehekea hii leo sikukuu ya Eid el Fitr.
Israel imesema Iran imeendelea kufyatua makombora mapema leo Jumamosi, huku Saudi Arabia ikisema imedungua droni 20 ndani ya saa kadhaa katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo, ambalo ni makazi ya mitambo mikubwa ya mafuta.
Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema hakukuwa na majeruhi wala uharibifu.