Trump aikosoa jumuiya ya kujihami ya NATO kuhusu Iran
9 Aprili 2026
Matangazo
Trump alisema amevunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuwa NATO haikuwepo wakati Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran.
Lakini Rutte kwa upande wake alisema alifanikiwa kuashiria ukweli kwamba idadi kubwa ya mataifa ya Ulaya yamekuwa yakisaidia katika kuweka kambi za kijeshi, uratibu na mipangilio, kwa kutumia ndege za ziada, na kuhakikisha yanatimiza ahadi zao.
Rutte alifanya mkutano wa faraghani na Trump kwa ajili ya majadiliano ambayo yalitarajiwa kuzingatia kuufungua tena mlango bahari wa Hormuz na kutuliza hasira ya Trump dhidi ya NATO kuhusu vita vya Iran.
Ikulu ya Marekani ilisema Trump angejadili uwezekano wa kuondoka katika muungano huo baada ya kushindwa kujiunga na vita hivyo.