1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aikosoa UN akisema imeshindwa kuleta amani duniani

24 Septemba 2025

Rais wa Marekani Donald ameukosoa Umoja wa Mataifa akisema umejaa maneno matupu na kwamba taasisi hiyo haisaidii katika kuleta amani ulimwenguni.

USA New York 2025 | Donald Trump akihutubia hadhara ya UN
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Jeenah Moon/REUTERS

Rais wa Marekani Donald Trump ameukosoa Umoja wa Mataifa akisema umejaa maneno matupu na kwamba taasisi hiyo haisaidii katika kuleta amani ulimwenguni. Trump ameyasema hayo wakati akihutubia viongozi wa dunia wanaohudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. Katika hotuba yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa shauku, Trump amesema taasisi ya Umoja wa Mataifa ina uwezo mkubwa wa kutatua migogoro lakini haijafanikiwa hata kidogo katika kutekeleza hilo.

Akijitamba kukomesha vita saba, Trump ameongeza kwamba katika hali zote hizo, Umoja wa Mataifa haukuweza hata kusaidia na kuhoji juu ya jukumu lake.

Rais Trump amelitumia jukwaa hilo kuelezea migogoro kadhaa, ikiwemo vita vya Gaza, mpango wa nyuklia wa Iran, suala la wahamiaji, vita vya Ukraine na mengineyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW