1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump aishinikiza NATO isitishe kununua mafuta ya Urusi

13 Septemba 2025

Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Jumuiya ya Kujihami ya NATO isitishe kununua mafuta ya Urusi na kuiwekea vikwazo vikubwa ili kuvimaliza vita nchini Ukraine. Ameitoa kauli hiyo kupitia barua aliyoiandika kwa NATO.

 Rais Donald Trump akiwa Ikulu ya Marekani, White house 2025
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: Mandel Ngan/AFP/Getty Images

Katika barua hiyo aliyoichapisha kwenye mitandao ya kijamii  13.09.2025 Trump ameeleza kuwa yuko tayari kuiwekea vikwazo Urusi kama mataifa wanachama wa Jumuiya hiyo yatakubali pia kufanya hivyo. Wito huo umetolewa wakati Urusi ikiendeleza vita vyake dhidi ya Ukraine ambapo imesema imefanikiwa kukidhibiti Kijiji cha Novomykolaivka katika mkoa wa Dnipropetrovsk. 

Licha ya madai ya Urusi, chanzo kutoka jeshi la Ukraine kimedai bado kijiji hicho kiko chini ya utawala wa Kyiv. Wizara ya Ulinzi ya Urusi imeeleza pia kuwa vikosi vyake vimezidungua droni 340 vya Ukraine katika siku moja iliyopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW