1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump ajitangaza mshindi wa urais Marekani

6 Novemba 2024

Matokeo ya awali yanaonesha Donald Trump anaongoza. Matokeo rasmi hayajatangazwa, lakini Donald Trump ameshajitangaza mshindi.

Donald Trump akizungumza huko Palm Beach mbele ya wafuasi wake
Donald Trump akizungumza huko Palm Beach mbele ya wafuasi wakePicha: Brendan McDermid/REUTERS

Matokeo ya awali yanaonesha Donald Trump anaongoza. Matokeo rasmi hayajatangazwa, lakini Donald Trump ameshajitangaza mshindi. Kura za uchaguzi wa urais Marekani zaendelea kuhesabiwa

Trump ametangaza kushinda urais akisema ni ushindi wa kihistoria ambao haujashuhudiwa nchini humo.

Kwenye hotuba mbele ya ushindi kwa wafuasi wake huko Palm Beach, Florida Trump aliyeongozana na familia yake, alikiri matokeo haya ni mabadiliko makubwa ya kisiasa na kuahidi kuliponya taifa hilo.

Donald Trump amewashukuru Wamarekani kwa heshima ya kumchagua kuwa Rais wa 45 na 47 wa nchi hiyo, akielekea kwenye ushindi katika uchaguzi wa kihistoria wa Marekani.

Mgombea mwenza wa Republican J.D VancePicha: Jim Watson/AFP/Getty Images

Trump ametangaza ushindi baada ya kushinda jimbo la Pennsylvania na kufikisha jumla ya kura 267 za wajumbe wa uchaguzi, akihitaji kura tatu kufikisha 270 zinazohitajika.Marekani yaamua: Chaguo ni kati ya Trump na Harris

Aliwaambia wafuasi wake kwamba huu ni ushindi mkubwa kwa watu wa Marekani, na utamruhusu kuifanya Marekani kuwa bora zaidi. Alitabiri kushinda kura 315 za Electoral College, ambazo zinapita 270 zinazohitajika kuwa Rais.

Trump alisema pia ameshinda kura za watu wa kawaida! Na moja ya mambo aliyozungumzia ni suala la uhamiaji. Amesema, 'Tutarekebisha mipaka yetu.'

Kuhusu mashambulizi ya maisha yake wakati wa kampeni, alisema, 'Mungu aliokoa maisha yangu kwa sababu, na hiyo ni kuokoa nchi yetu na kuirejesha kwenye ukuu.'