1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Trump akana mashitaka yanayohusiana na uchaguzi

4 Agosti 2023

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amekana mashitaka ya jinai yanayomkabili, kwamba alikula njama ya kutaka kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 na kuwalaghai Wamarekani.

USA Washington D.C Ankunft Trump Gerichtstermin
Picha: Alex Brandon/AP Images

Trump ambaye anaoongoza katika uteuzi wa wagombea urais mwaka 2024 ndani ya Republican, alikana makosa hayo wakati kesi dhidi yake ilipokuwa ikisikilizwa katika mahakama ya mjini Washington.

Soma pia: Trump ashtakiwa kwa kutaka kubatilisha matokeo ya 2020

Mwendesha mashitaka maalum Jack Smith alimshutumu Trump na washirika wake kwa kuendeleza madai ya uongo kuwa uchaguzi uligubikwa na udanganyifu na kushinikiza maafisa wa majimbo na shirikisho kubadilisha matokeo.

Bilionea huyo mwenye umri wa miaka 77 tayari amefunguliwa mashtaka katika kesi nyingine mbili za jinai, huku mashtaka hayo mapya ya kula njama yakiongeza uwezekano wa Trump kuhusishwa zaidi kwenye michakato ya kisheria wakati wa kilele cha kampeni za uchaguzi wa mwaka ujao.