1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akataza usafiri kwenda na kutoka Ulaya kuzuwia corona

Sekione Kitojo
12 Machi 2020

Rais Donald Trump  wa  Marekani amekataza safari zote kutoka Ulaya kwenda Marekani kwa siku 30, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuzuwia  usambaaji wa  janga la  virusi  vya  corona. 

US-Präsident Trump spricht über die Reaktion der USA auf die COVID-19-Coronavirus-Pandemie
Picha: Reuters/D. Mills

Wakati  huo huo  Umoja  wa  Ulaya  utafanya  tathmini  yake  kuhusu  marufuku hiyo  ya  kusafiri  iliyowekwa  na  Rais Trump, amesema  rais  wa baraza  la  Ulaya  Charles Michel, na  kuongeza  kwamba  mvurugiko wa kiuchumi ni  lazima  uepukwe. 

Marufuku  iliyowekwa  na  Rais Donald Trump  ya  kusitisha usafiri kutoka  mataifa  ya  Umoja  wa  Ulaya isipokuwa Uingereza  inaanza rasmi  usiku  wa  manane  siku  ya  Ijumaa, lakini  haitajumuisha wasafiri  kutoka  Uingereza, ambayo  imejiondoa  kutoka  Umoja  wa Ulaya  hivi  karibuni, amesema   rais  huyo. Trump akilihutubia  taifa kutoka  katika  ofisi  ya  rais katika  ikulu  ya  White House  alisema.

"Baada  ya  kushauriana  na  maafisa  wetu  wa  juu wa  afya ,nimeamua  kuchukua  hatua  kali lakini  muhimu  ili  kulinda  afya  na hali  ya  Wamarekani  wote. Kuzuwia  maambukizi  mapya  kuingia katika  nchi  yetu tutasitisha  kwa  muda  safari  zote  kutoka  Ulaya kwenda  Marekani  katika  muda  wa  siku 30 zijazo. Sheria  hizi mpya  zitaanza  kazi usiku  wa  manane ijumaa."

Katika  hotuba  hiyo  kwa  taifa  hilo  ambalo  liliingiwa  na  hofu, Trump  ametaka  kupuuzia  wakosoaji  ambao  wanasema  utawala wake  umekosekana  katika  wakati  huu  wa  mzozo, akisisitiza kuwa "virusi  havitakuwa  na  nafasi nchini  humo."

Rais wa baraza la Ulaya Charles Michel Picha: Reuters/F. Lenoir

Amesema  kuwa , "hizi ni  juhudi  za  nguvu  na  sahihi  kudhibiti virusi kutoka  nje  katika  historia  ya hivi  sasa:"

Ametangaza  hatua  kadhaa  kupunguza  mzigo  wa  kifedha  kwa watu  ambao  watalazimika  kuwamo  katika  mapumziko kwa  wiki kadhaa  wakiwa  katika  karantini.

Lakini  tangazo  lake  kubwa  linalofika  mbali  ni  kusitisha  usafiri kwenda  na  kutoka  Ulaya , na  hili  limeleta  hali  ya  mkanganyiko mkubwa  wakati  akisikika  kimakosa  kwamba  anasitisha  pia biashara  kati  ya  Marekani  na  Ulaya.

Ikulu  ya  Marekani  baadaye  ilifafanua  kuwa  bidhaa  zitaendelea kuingia  nchini  humo  kutoka  Ulaya. Trump  alionekana  kuilaumu Ulaya  katika  jukumu  la  kusambaa  kwa  virusi , ambavyo vilijitokeza  kwanza  nchini  China na  kwa  sasa  vimesambaa duniani kote, na  kusababisha  ishara  hatari  za  kama  mafua.

Udhibiti wa virusi vya Corona katika viwanja vya ndegePicha: AFP/Salvadorean Presidency

Mataifa  ya  Umoja  wa  Ulaya  yatafanya  tathmini  leo  kuhusu marufuku  hiyo  iliyotangazwa  na  rais Trump, rais wa  baraza  la Umoja  huo Charles Michel  amesema  na  kuongeza  kwamba uvurugaji  wa   uchumi  unapaswa  kuepukwa.

Ulaya  inachukua   kila  aina  ya  hatua  kudhibiti kusambaa  kwa virusi  vya  COVID-19, kupunguza  idadi  ya  maambukizi na  kutoa msaada  kwa  ajili  ya  utafiti, amesema  Michel.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW