1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akosolewa kwa kuashiria kuzitwaa Greenland, Canada

8 Januari 2025

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amezuwa tafrani ya kimataifa baada ya kutaja uwezekano wa kuuchukuwa Mfereji wa Panama, kisiwa cha Greenland na kuigeuza Canada kuwa jimbo la 51 la nchi yake.

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump.
Rais mteule wa Marekani, Donald Trump.Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Fllorida hapo jana, alisema hawezi kuondosha uwezekano wa kutumia nguvu za kiuchumi au kijeshi kutwaa udhibiti wa Mfereji wa Panama na Greenland.

Kwa upande mwengine, Trump alikosowa vikali utumiaji wa bidhaa za Canada na pia msaada wa kijeshi wa Marekani kwa jirani yake huyo, akidai mpaka baina yao ni wa kubuni.

Soma zaidi: Trump bado anakabiliwa na hukumu ya kumlipa kahaba

Kuhusu Greenland, kisiwa chenye utajiri wa rasilimali kinachomilikiwa na Denmark, Trump alisema atatumia shinikizo la kiuchumi ikiwa Copenhagen itakataa kuiuzia Marekani kisiwa hicho.

Waziri Mkuu wa Canada, Justin Treudau, amemkosowa vikali Trump kwa kauli yake hiyo, huku Panama ikisema hakuna namna yoyote ambapo itayatowa mamlaka yake kwa Marekani.

Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen, amesema kisiwa cha Greenland hakiko kwenye mnada.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW