1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump akutana na Rais Zelensky mjini New York

27 Septemba 2024

Mgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican, Donald Trump, amekutana kwa mazungumzo na Rais Volodymyr Zelensky mjini New York.

Donald Trump alipokutana na Volodymyr Zelensky
Donald Trump alipokutana na Volodymyr ZelenskyPicha: Alex Kent/Getty Images

Mgombea wa urais wa Marekani kwa tikiti ya chama cha Republican, Donald Trump, amekutana jioni hii kwa mazungumzo na Rais Volodymyr Zelensky, siku moja baada ya kumshambulia kiongozi huyo wa Ukraine kwa kukataa kufikia makubaliano ya kumaliza vita na Urusi. Marekani yaimwagia mabilioni Ukraine kuongeza nguvu uwanja wa vita

Mkutano baina ya wawili hao unafanyika kwenye jengo la hoteli ya fahari inayomilikiwa na rais huyo wa zamani lililopo mjini New York.

Zelensky, ambaye yuko nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa, tayari alikutana jana Alhamisi na Rais Joe Biden pamoja na mgombea urais kupitia chama cha Democratic, Kamala Harris.

Hapo jana Trump alisema kile kinachoendelea nchini Ukraine ni "jambo la aibu na kuhuzunisha" kutokana vifo na uharibifu unaosababishwa na vita.Zelensky: Urusi inapanga kushambulia mitambo yetu ya nyuklia

Amesema anaamini anao uwezo wa kufikia makubaliano yatakayomaliza vita hivyo vilivyozuka baada ya Urusi kuivamia kijeshi Ukraine mwaka 2022.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW