1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump amemteua Kash Patel kama mkurugenzi mpya wa FBI

1 Desemba 2024

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amemteua Kash Patel, wakili na mkosoaji mkubwa wa shirika la upelelezi wa ndani la Marekani (FBI) kama mkurugenzi ajae. Mteule huyo pia alikuwa anapinga muundo wa shirika hilo.

Kash Patel
Kash Patel, mkuu wa zamani wa wafanyikazi akizungumza katika mkutano wa hadhara huko Minden, Nv., Oct. 8, 2022Picha: José Luis Villegas/AP Photo

Katika taarifa aliyoichapisha katika mtandao wa kijamii, Trump alimuelezea Patel kama "wakili mahiri, mpelelezi na mtoa kipaumbele katika maslahi ya Marekani. Patel amefanya kazi katika Kamati ya Intelijensia ya Bunge la Marekani, ambapo alikuwa na wajibu muhimu katika uchunguzi wa madai ya Urusi katika kuuingilia uchagui wa rais wa 2016. Patel, anayejulikana kwa utiifu wake thabiti kwa Trump, alihudumu katika majukumu muhimu wakati wa utawala wa kwanza wa Trump, ikiwa ni pamoja na kitengo cha kusimamia kukabiliana na ugaidi katika Baraza la Usalama la Taifa na baadaye akihudumu kama mkuu wa wafanyakazi katika Idara ya Ulinzi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW