1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump ampongeza Putin kwa ridhaa ya kubadilishana wafungwa

4 Agosti 2024

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump amempongeza Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kufanikisha moja kati ya makubaliano makubwa ya kubadilishana wafungwa kati ya Urusi, Belarus na mataifa mengine kadhaa ya Magharibi.

Marekani Cleveland | Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump alipopatikana na hatia katika makosa yote 34 ya kughushi rekodi za biashara. Mei 30 2024.Picha: Dennis Van Tine/STAR MAX/IP/zz/picture alliance / zz/Dennis Van Tine/STAR MAX/IPx

Akizungumza katika jukwaa la kampeni mjini Atlanta, jimboni Georgia Trump amesema pamoja na kwamba hata baadhi ya watu waouvu wamepata nafasi ya kuwa huru, Marekani imefanikiwa pia kurejeshewa watu wake.

Katika kile kinachoonekana kama ubadilishanaji wa wafungwa ambao haujawahi kutokea, Urusi na Belarus ziliwaachilia huru watu 16 ambao walifungwa kutokana na shughuli zao kama waandishi wa habari na wanaharakati, miongoni mwa mambo mengine.

Makubialiano hayo ya kubadilisha wafungwa yalihusisha kuachiliwa kwa wafungwa wengine 10 kurejea Urusi kutoka katika magereza ya mataifa mbalimbali ya Magharibi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW