1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump amuomba Rais wa Israel kutoa msamaha kwa Netanyahu

13 Novemba 2025

Rais wa Israel Isaac Herzog, amepokea barua kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump, ikimuhimiza kufikiria kutoa msamaha kwa Waziri Mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu.

USA Washington D.C. 2025 | Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump amuomba Rais wa Israel kutoa msamaha kwa Benjamin NetanyahuPicha: Jonathan Ernst/REUTERS

Netanyahu amekuwa akikabiliwa na kesi ya muda mrefu ya ufisadi na Trump kwa mara kadhaa amekuwa akimuombea msamaha kwa washirika wake wa karibu. Netanyahu hata hivyo, amekanusha madai yanayomkabili na kusema hana hatia.

Katika barua hiyo Trump alisema anaheshimu uhuru wa mfumo wa sheria nchini Israel, lakini anaamini kwamba kesi hiyo dhidi ya Netanyahu, ni ya kisasa zaidi na isiyo ya msingi.

Ofisi ya rais imesema mtu yeyote anayetaka msamaha wa rais ni lazima awasilishe ombi rasmi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.

Muda mfupi baada ya barua hiyo kufikishwa kwa Herzog, Netanyahu aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akimshukuru Trump kumuunga mkono, akisema anatarajia kuendelea na ushirikiano wao kuimarisha usalama na amani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW