1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Trump anaanza ziara ya kitaifa nchini Uingereza

17 Septemba 2025

Rais Donald Trump wa Marekani anafanya ziara ya pili ya kitaifa nchini Uingereza leo Jumatano ambayo watawala mjini London wanatumai itasaidia kuimarisha mahusiano na Washington.

Uingereza London 2025 | Donald Trump na Melania Trump wakiwasili nchini Uingereza
Rais Donald Trump wa Marekani na mkewe Melania wakiwasili nchini Uingereza Jumanne, Septemba 16, 2025.Picha: Alastair Grant/AP Photo/picture alliance

Trump aliyewasili Uingereza Jumanne jioni akifuatana na mkewe Melania, atakaribishwa na Mfalme Charles III kwenye kasri la Windsor kwa halfa ya fahari itakayojumuisha heshima ya zulia jekundu, gwaride la kijeshi na dhifa ya chakula cha jioni.

Kwa desturi, Uingereza huwakaribisha viongozi wa kigeni kufanya ziara moja pekee ya kitaifa na Trump alipata heshima hiyo mwaka 2019 alipoalikwa kuitembelea Uingereza na Malkia Elizabeth II.

Hata hivyo ziara hii nyingine ambayo si ya kawaida inazingatiwa kuwa sehemu ya mkakati wa Uingereza wa kumweka karibu kiongozi huyo anayejulikana kwa sera zisizotabirika.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW